Saturday, October 5, 2013

J - MARTINS AWAPAGAWISHA MASHABIKI WA TANGA ,KATIKA TAMASHA LA FIESTA

pichani juu na chini ni Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria,J-Mrtin akitumbuiza jukwaani usiku wa leo,kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,ambaye pia ni mtoto wa Mkongwe wa muziki wa dansi hapa nchini,Mzee Zorro,Maunda Zorro akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu kwenye uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga wakati tamasha la Serengeti fiesta 2013 likiendelea.
Mzee wa Masauti,Christian Bella akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu ndani ya uwanja wa Mkwakwani
Sehemu ya mashabiki wakishangweka huku manyunyu ya mvua yakisumbua hapa na pale usiku huu.span>
Mkali mwingine wa miondoko ya mitindo huru,God Zilla akishusha mistari yake mbele ya mashabiki wake waliokuwa wakiitikia kwa pamoja,ndani ya uwanja wa mkwakwani usiku huu wakati tamasha la serengeti fiesta likiendelea,sambamba na hali ya hewa ya mvua mvua huku mashabiki wakiendelea kupiga mayowe na miluzi kila kona ya uwanja.
Mwanadada Linah ambaye anafanya vyema katika ya muziki wa Bongofleva akicheza na shabiki wake jukwaani.
Msanii ambaye ni muigizaji lakini pia anasumbua sana katika anga ya muziki wa bongofleva,Shilole sambamba na skwadi lake wakilishambulia vilivyo jukwaa usiku huu wakati tamasha la serengeto fiesta likiendelea ndani ya uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga. Picha zaidi nenda Jiachie Blog

Sunday, August 18, 2013

RWANDA KATIKA TASWIRA

Wabongo tuna kasafari karefu kidogo kwa upande wa Miundombinu, Vijana tusilale,bado mapambano

Friday, August 9, 2013

Alichokisema Lulu kuhusu ishu ya elimu na mastaa wa bongo


luluxShule ni kitu cha msingi sana kwa mtu yoyote hasa yule ambaye ni kioo cha jamii au kiongozi. Sasa muigizaji Lulu amechukua hatua zake kwenye hii ishu ya elimu pamoja na kusema maneno,”Gettin more knowledge…..!!!we have to learn….especially sisi celebrities wa bongo….wengi wetu tunaongeaga pumba sana in public…yan hatujui nini tuongee wapi!!!!juc an advice lakni…..!!!!AM GOOD TO GO….”

Thursday, July 4, 2013

NDEGE WA TATU (NDEGE 3) NI KUNDI JIPYA JIJINI DAR ES SALAAM

Kutoka kushoto ni Paulyne Zongo, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Joan Matovolwa.Wanamuziki hao watatu na wakongwe nchini ndio wanaounda kundi hilo litakalojulikana kwa jina la NDEGE 3
Kundi la Ndege 3 linaloundwa na wanamuziki wakongwe katika Tasnia ya muziki wa dansi na kizazi kipya Joan matovolwa, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Paulyne Zongo, hivi karibuni limeshatoa kibao chake kinachokwenda kwa jina la 'MISUKOSUKO YA MAPENZI' ambacho redio kadhaa nchini zimeanza kukirusha.
 
MISUKOSUKO YA MAPENZI ni nyimbo ambayo imetungwa kwa umahiri wa hali ya juu, na kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji na utunzi.
 
Kwa sasa Joan Matovolwa na Paulyne Zongo ni wanamuziki huru wakati Khadija Mnoga (Kimobitel) ni mwanamuziki anayeimba katika bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Camarade Ally Choki.

Friday, June 14, 2013

PICHA ZA KALA JEREMIAH AKITOA TUZO YAKE YA HIP HOP KWA MAMA WA MANGWEA




Mama mzazi wa marehemu Albert Mangweha akiwa ameshikilia tuzo aliyopewa kwa niaba ya mwanae, tuzo hii aliipata msanii Kala Jeremiah kwenye tuzo za Kilimanjaro ikiwa kama tuzo ya msanii bora ya Hip Hop 2013-14