Kutoka
kushoto ni Paulyne Zongo, Khadija Mnoga (Kimobitel) na
Joan Matovolwa.Wanamuziki hao watatu na wakongwe nchini ndio wanaounda
kundi hilo litakalojulikana kwa jina la NDEGE 3
Kundi
la Ndege 3
linaloundwa na wanamuziki wakongwe katika Tasnia ya muziki wa dansi na
kizazi kipya Joan matovolwa, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Paulyne Zongo,
hivi karibuni limeshatoa kibao chake kinachokwenda kwa jina la
'MISUKOSUKO YA MAPENZI' ambacho redio kadhaa nchini zimeanza kukirusha.
MISUKOSUKO
YA MAPENZI ni nyimbo ambayo imetungwa kwa umahiri wa hali ya juu, na
kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji na utunzi.
Kwa
sasa Joan Matovolwa na Paulyne Zongo ni wanamuziki huru wakati Khadija
Mnoga (Kimobitel) ni mwanamuziki anayeimba katika bendi ya Extra Bongo
inayoongozwa na Camarade Ally Choki.