Thursday, July 4, 2013

NDEGE WA TATU (NDEGE 3) NI KUNDI JIPYA JIJINI DAR ES SALAAM

Kutoka kushoto ni Paulyne Zongo, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Joan Matovolwa.Wanamuziki hao watatu na wakongwe nchini ndio wanaounda kundi hilo litakalojulikana kwa jina la NDEGE 3
Kundi la Ndege 3 linaloundwa na wanamuziki wakongwe katika Tasnia ya muziki wa dansi na kizazi kipya Joan matovolwa, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Paulyne Zongo, hivi karibuni limeshatoa kibao chake kinachokwenda kwa jina la 'MISUKOSUKO YA MAPENZI' ambacho redio kadhaa nchini zimeanza kukirusha.
 
MISUKOSUKO YA MAPENZI ni nyimbo ambayo imetungwa kwa umahiri wa hali ya juu, na kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji na utunzi.
 
Kwa sasa Joan Matovolwa na Paulyne Zongo ni wanamuziki huru wakati Khadija Mnoga (Kimobitel) ni mwanamuziki anayeimba katika bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Camarade Ally Choki.

0 comments:

Post a Comment