Msanii
Mkongwe wa Luninga na Vichekesho nchini Tanzania Asha Boko anategemea
kuachia Video yake ya Kibonge Mnene mwisho wa mwezi huu. Video hiyo
ambayo Audio yake ilifanyika katika Studio ya Kwanza Records iliyopo
Morogoro imetayarishwa na Fasdo Video.Kwanza Records ni moja ya studio
bora nchini Tanzania ambayo imekuwa ikisaidia kuinua vipaji vy muziki wa
Bongo Fleva. Kwa wale wanaokumbuka Kwanza Records kwa mara ya Kwanza
iliweza kumtambulisha Msanii Kitale aliyomshirikisha Marehemu Sharo
Milionea iitwayo Hili Dude Noma.
Akiongea
na Timu ya Mwaipaja Blog, Asha Boko amesema kuwa wadau wa Muziki wa
Bongo Fleva wakae mkao wa kula kwakuwa amefanya mambo makubwa ndani ya
Video hiyo.Asha Boko ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza kufanya
naye kazi ikiwemo filamu, movie na Bongo Fleva.
Kwa
watakaohitaji kuwasiliana na Asha Boko wawasiliane nae kwa namba yake
ya mkononi ambayo ni 0754 273904 ila wasibip wala kumwomba Vocha