Sunday, May 5, 2013

MAGWIJI KUKINUKISHA MJI KASORO BAHARI

Wanamuziki mahiri kutoka studio za kwanza records,wamezidi kuwa gumzo ndani ya mkoa wa Morogoro kutokana na uwezo na vipaji walivyonavyo.Wanamuziki hao ambao ni Mycoely(kushoto) pamoja Kenny(kulia) kama wanavyoonekana kwenye picha,wanauwezo mkubwa wa kuimba na kupiga gitaa kwa wakati mmoja ambapo wamekuwa kivutio kikubwa machoni na masikioni mwa watu wengi,wanawaahidi mashabiki wao wakae mkao wa kula,kwani kuna mengi ambayo wameaandalia ndani ya mwaka huu.