Msemaji
wa Kamati ya Mazishi ya Marehemu Albert Mangwea ambaye pia ni Director
kutoka Visual lab Bw Adam Juma akielezea ratiba ya Shughuli nzima ya
Mazishi itakavyokuwa mara baada ya zoezi la kutoa heshima za mwisho
zitakapomalizika
Baadhi
ya Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Wa Kwanza Kabisa ni Mkoloni
akifuatiwa na Madee ambaye ni wa Tatu kutoka Mbele wakitoa heshima zao
za mwisho kwa mwili wa Marehemu Albert Mangwea
Msanii Wa Muziki wa Kizazi Kipya Nasibu Abdul almaarufu kama Diamond akipita kutoa heshima zake za mwisho.
Baadhi
ya Wasanii wa Fani mbalimbali pamoja na ndugu,jamaa na marafiki
wakipita pembezoni mwa jeneza lililobeba mwili wa Marehemu Albert
Mangwea na kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Albert Mangwea leo
katika viwanja vya leaders
Msanii
wa Muziki Keisha (aliyejifunga kiremba Cheupe) akifuatiwa na Noora
wakiwa na nyuso za huzuni wakati wakipita kwaajili ya kutoa heshima zao
za mwisho katika viwanja vya leaders
Wasanii
wa fani ya Maigizo hapa Nchini Mzee Magari (aliyeshika Koti jeusi)
akifuatiwa na Msanii Natasha Pamoja na Monalisa wakipita kwaajili ya
Kutoa Heshima zao Za mwisho kwa Marehemu Albert Mangweha leo katika
Viwanja vya leaders
Baadhi ya Ndugu, Jamaa na Marafiki wakitoa Heshima za Mwisho
Jeneza
lenye Mwili wa Marehemu Albert Mangweha likiwa juu ya meza tayari kwa
Wakazi wa Jiji la Dar Kuanza kutoa Heshima Zao za Mwisho katika Viwanja
Vya Leaders.
Mwakilishi
kutoka Wizara ya Habari, utamaduni na Michezo Bi Lilian Bereko akitoa
Salamu za Rambirambi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo leo
katika viwanja vya leaders kabla ya Wakazi wa Jiji la Dar hawajaanza
kutoa heshima zao za mwisho