Thursday, March 21, 2013

SIKU YA UZINDUZI WA ALBAM YA LADY JAY DEE "JOTO HASIRA" DAR ES SALAAM

Mkongwe wa Muziki wa Kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo maarufu kama Lady Jaydee alifanya uzinduzi wa video yake mpya juzi ,aliyomshirikisha Mkongwe Mwenzake wa muziki wa kizazi kipya Bw. Joseph Haule ‘Prof. J’  kwenye Video ya Wimbo huo wa "JOTO HASIRA"

Pichani juu ni Lady Jaydee akiimba wimbo wake huo mpya wa Joto Hasira kwaheri shida, mbele ya mashabiki wake wakati wa uzinduzi wa video ya wimbo huo.
 
Jaydee alifanya uzinduzi huo katika mgahawa wake wa Nyumbani Lounge uliopo Namanga wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mamia ya wapenzi wa Burudani na muziki wa mwana dada huyo.

Uzinduzi huo ulisindikizwa na bendi ya Lady Jaydee ya Machozi Band na kutoa burudani ambayo ilikonga nyoyo za mashabiki wake.
Jaydee akiwa kando ya gari lake mara baada ya kuwasili Nyumbani Lounge tayari kwaajili ya uzinduzi wa Video yake mpya ya Joto Hasira.
Lady JayDee akitoa burudani mbele ya mashabiki wake
Vyombo mbali mbali vya habari  vikipata mawili matatu kutoka kwa Komandoo Jide ndni ya Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam.
Hapa Lady Jay Dee akifanya mahojiano na mtangazaji mahiri wa clouds fm Millard Ayo
Gadner G. Habash ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa Nyumbani Lounge na Machozi Band akizungumza na vijana walioshiriki katika kutengeneza Video mpya ya Joto Hasira ya Lady JayDee
 Prof.J ameshiriki katika wimbo huo wa Lad JayDee Joto Hasira nae alikuwepo Ukumbini hapo, hapa akipiga picha na Warembo walio pamba show hiyo.
Shangwe Za kutosha kwa Komandoo Jide
Wana dada waandishi wa habari waki show love katika uzinduzi wa wimbo wa Lady Jay Dee "JOTO HASIRA"