Mkongwe
wa Muziki wa Kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo maarufu kama Lady Jaydee alifanya uzinduzi wa video yake mpya juzi ,aliyomshirikisha Mkongwe
Mwenzake wa muziki wa kizazi kipya Bw. Joseph Haule ‘Prof. J’ kwenye Video ya Wimbo huo wa "JOTO HASIRA"
Pichani juu ni Lady Jaydee akiimba wimbo wake huo mpya wa Joto Hasira kwaheri shida, mbele ya mashabiki wake wakati wa uzinduzi wa video ya wimbo huo.
Jaydee
alifanya uzinduzi huo katika mgahawa wake wa Nyumbani Lounge uliopo Namanga
wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mamia ya wapenzi wa
Burudani na muziki wa mwana dada huyo.
Uzinduzi
huo ulisindikizwa na bendi ya Lady Jaydee ya Machozi Band na kutoa burudani
ambayo ilikonga nyoyo za mashabiki wake.
Jaydee akiwa kando ya gari lake mara
baada ya kuwasili Nyumbani Lounge tayari kwaajili ya uzinduzi wa Video yake
mpya ya Joto Hasira.
Lady JayDee akitoa burudani mbele ya
mashabiki wake
Vyombo mbali mbali vya habari vikipata mawili matatu kutoka kwa Komandoo Jide ndni ya Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam. |
Gadner G.
Habash ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa Nyumbani Lounge na Machozi Band
akizungumza na vijana walioshiriki katika kutengeneza Video mpya ya Joto Hasira
ya Lady JayDee
Prof.J
ameshiriki katika wimbo huo wa Lad JayDee Joto Hasira nae alikuwepo
Ukumbini hapo, hapa akipiga picha na Warembo walio pamba show hiyo.
Shangwe Za kutosha kwa Komandoo Jide |
Wana dada waandishi wa habari waki show love katika uzinduzi wa wimbo wa Lady Jay Dee "JOTO HASIRA" |
0 comments:
Post a Comment