skip to main |
skip to sidebar
J - MARTINS AWAPAGAWISHA MASHABIKI WA TANGA ,KATIKA TAMASHA LA FIESTA
pichani juu na chini ni
Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria,J-Mrtin akitumbuiza jukwaani usiku wa
leo,kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Mkwakwani
mkoani Tanga.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi
kipya,ambaye pia ni mtoto wa Mkongwe wa muziki wa dansi hapa nchini,Mzee
Zorro,Maunda Zorro akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu kwenye uwanja
wa Mkwakwani mkoani Tanga wakati tamasha la Serengeti fiesta 2013
likiendelea.
Mzee wa Masauti,Christian Bella akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu ndani ya uwanja wa Mkwakwani
Sehemu ya mashabiki wakishangweka huku manyunyu ya mvua yakisumbua hapa na pale usiku huu.span>
Mkali mwingine wa miondoko ya
mitindo huru,God Zilla akishusha mistari yake mbele ya mashabiki wake
waliokuwa wakiitikia kwa pamoja,ndani ya uwanja wa mkwakwani usiku huu
wakati tamasha la serengeti fiesta likiendelea,sambamba na hali ya hewa
ya mvua mvua huku mashabiki wakiendelea kupiga mayowe na miluzi kila
kona ya uwanja.
Mwanadada Linah ambaye anafanya vyema katika ya muziki wa Bongofleva akicheza na shabiki wake jukwaani.
Msanii ambaye ni muigizaji lakini
pia anasumbua sana katika anga ya muziki wa bongofleva,Shilole sambamba
na skwadi lake wakilishambulia vilivyo jukwaa usiku huu wakati tamasha
la serengeto fiesta likiendelea ndani ya uwanja wa Mkwakwani mkoani
Tanga. Picha zaidi nenda Jiachie Blog
0 comments:
Post a Comment