Tuesday, May 7, 2013

Ngoma kali kutoka Kwanza Records


G Nako ft Ben pol - Mama Yeyoo


Cheki video,Chidi benz alivyodundwa na Kalapina ndani ya maisha club!


KWANZA RECORDS MGODI WA VIPAJI

Kutana na mwanamuziki mahili wa miondoko ya Hip Hop,mwenye uwezo mkubwa na mwaunye mashairi ya kibaba,ambaye amewahi kuwa super nyota wa Fiesta mwaka jana.Joh Maker ndio jina lake la biashara,ambaye anatarajia kuachia bonge ya ngoma hivi karibuni,usiache kutembelea blog hii ili upate habari nyingi zaidi kumuhusu yeye.

Sunday, May 5, 2013

MAGWIJI KUKINUKISHA MJI KASORO BAHARI

Wanamuziki mahiri kutoka studio za kwanza records,wamezidi kuwa gumzo ndani ya mkoa wa Morogoro kutokana na uwezo na vipaji walivyonavyo.Wanamuziki hao ambao ni Mycoely(kushoto) pamoja Kenny(kulia) kama wanavyoonekana kwenye picha,wanauwezo mkubwa wa kuimba na kupiga gitaa kwa wakati mmoja ambapo wamekuwa kivutio kikubwa machoni na masikioni mwa watu wengi,wanawaahidi mashabiki wao wakae mkao wa kula,kwani kuna mengi ambayo wameaandalia ndani ya mwaka huu.

Thursday, March 21, 2013

SIKU YA UZINDUZI WA ALBAM YA LADY JAY DEE "JOTO HASIRA" DAR ES SALAAM

Mkongwe wa Muziki wa Kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo maarufu kama Lady Jaydee alifanya uzinduzi wa video yake mpya juzi ,aliyomshirikisha Mkongwe Mwenzake wa muziki wa kizazi kipya Bw. Joseph Haule ‘Prof. J’  kwenye Video ya Wimbo huo wa "JOTO HASIRA"

Pichani juu ni Lady Jaydee akiimba wimbo wake huo mpya wa Joto Hasira kwaheri shida, mbele ya mashabiki wake wakati wa uzinduzi wa video ya wimbo huo.
 
Jaydee alifanya uzinduzi huo katika mgahawa wake wa Nyumbani Lounge uliopo Namanga wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mamia ya wapenzi wa Burudani na muziki wa mwana dada huyo.

Uzinduzi huo ulisindikizwa na bendi ya Lady Jaydee ya Machozi Band na kutoa burudani ambayo ilikonga nyoyo za mashabiki wake.
Jaydee akiwa kando ya gari lake mara baada ya kuwasili Nyumbani Lounge tayari kwaajili ya uzinduzi wa Video yake mpya ya Joto Hasira.
Lady JayDee akitoa burudani mbele ya mashabiki wake
Vyombo mbali mbali vya habari  vikipata mawili matatu kutoka kwa Komandoo Jide ndni ya Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam.
Hapa Lady Jay Dee akifanya mahojiano na mtangazaji mahiri wa clouds fm Millard Ayo
Gadner G. Habash ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa Nyumbani Lounge na Machozi Band akizungumza na vijana walioshiriki katika kutengeneza Video mpya ya Joto Hasira ya Lady JayDee
 Prof.J ameshiriki katika wimbo huo wa Lad JayDee Joto Hasira nae alikuwepo Ukumbini hapo, hapa akipiga picha na Warembo walio pamba show hiyo.
Shangwe Za kutosha kwa Komandoo Jide
Wana dada waandishi wa habari waki show love katika uzinduzi wa wimbo wa Lady Jay Dee "JOTO HASIRA"

Wednesday, March 6, 2013

HEMEDI,TIMBULO,ROSE NDAUKA NA MZEE CHILO KUTOKA NA MOVIE YA WORLD OF BENEFIT

 Sehemu ya Movie ya World of Benefit


 Maandalizi ya utayarishaji wa Movie.




Wasanii wakiwa location kwa ajili ya Movie mpya ya WORLD OF BENEFIT.

Picha kwa hisani ya Mcddenis Mgatha