Kwanza Records ni studio ya kisasa iliyopo Morogoro mjini ambayo kazi zake zimekuwa zikifanya vizuri katika uimwengu wa muziki wa kizazi kipya. Kwa mara ya Kwanza Studio ya Kwanza Records ilifanikiwa kumtambulisha katika anga la Muziki wa Bongo Fleva Msanii na Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania ajulikanaye kwa jina la Kitale akimshirikisha msanii mwenzake ambaye kwa sasa ni marehemu, namzungumzia Sharo Milionea.
Wasanii hao kwa pamoja waliweza kutengeneza nyimbo nzuri na inayopendwa na wengi ijulikanayo kama HILI DUDE NOMA., Nyimbo hiyo imekuwa gumzo katika anga la muziki wa kitanzania. Kwa faida ya wapenzi wa Blog hii, mwasisi wa Studio ya Kwanza Records ni Amani Mwaipaja. Lengo kuu la studio ya Kwanza Records ni kusaidia vijana wa kitanzania kukuza vipaji vyao kupitia sanaa ya muziki hasa wasanii watokao mikoani.
Mpaka sasa, baadhi tu ya wasanii walioweza kutoka kupitia studio ya Kwanza Records ni pamoja na:
Kitale na Sharo Milionea (jina la wimbo-Hili dude noma)
Asha Boko (jina la wimbo-Kibonge Mnene)
Joh Maker (Mshindi wa Fiesta Nyota akiwakirisha Mkoa wa Morogoro 2012)
Mash J (Mshiriki wa Fiesta Nyota 2012 kutokea Morogoro)
Afande Sele (jina la wimbo-Mashikolo Mageni)
Ballet Wallet (jina la wimbo-Mr. President)
Kenedy Masanja (jina la wimbo-Kamba Ndefu)
Sesilia Saleko (jina la wimbo-Kwepa Uterezi)
Sifuni Kwaya (Wamefanya albam nzima)
Mao Thobias (jina la wimbo-Kinywa)
Levina Stiven (jina la wimbo-Usikate tamaa)
J-Zinga jina la wimbo-Kibena)
Mycoel (jina la wimbo Rudi)
Vent Skills (jina la wimbo-Stay away)
Swahili Genge (jina la wimbo-Red Card)
Man Gao (jina la wimbo-Mama watoto)
Man 2C (jina la wimbo-mzee wa kitaa)
Jacca (jina la wimbo-mbiu ya mnyonge)
Bon Face (jina la Wimbo-Bado mtoto)
Mide Zoo
Kwa ujumla list ya wasanii waliopitia kwanza Records ni kubwa na inazidi kuongezeka kila kukicha.Studio ya Kwanza Records ipo chini ya Producer Vent Skills na sasa Kwanza Records inamtambulisha kwenu Msanii Mycoel,Tafadhalini Mpokeeni Kwa mawasiliano piga 0653 361 070
0 comments:
Post a Comment