Thursday, March 21, 2013

SIKU YA UZINDUZI WA ALBAM YA LADY JAY DEE "JOTO HASIRA" DAR ES SALAAM

Mkongwe wa Muziki wa Kizazi kipya, Judith Wambura Mbibo maarufu kama Lady Jaydee alifanya uzinduzi wa video yake mpya juzi ,aliyomshirikisha Mkongwe Mwenzake wa muziki wa kizazi kipya Bw. Joseph Haule ‘Prof. J’  kwenye Video ya Wimbo huo wa "JOTO HASIRA"

Pichani juu ni Lady Jaydee akiimba wimbo wake huo mpya wa Joto Hasira kwaheri shida, mbele ya mashabiki wake wakati wa uzinduzi wa video ya wimbo huo.
 
Jaydee alifanya uzinduzi huo katika mgahawa wake wa Nyumbani Lounge uliopo Namanga wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mamia ya wapenzi wa Burudani na muziki wa mwana dada huyo.

Uzinduzi huo ulisindikizwa na bendi ya Lady Jaydee ya Machozi Band na kutoa burudani ambayo ilikonga nyoyo za mashabiki wake.
Jaydee akiwa kando ya gari lake mara baada ya kuwasili Nyumbani Lounge tayari kwaajili ya uzinduzi wa Video yake mpya ya Joto Hasira.
Lady JayDee akitoa burudani mbele ya mashabiki wake
Vyombo mbali mbali vya habari  vikipata mawili matatu kutoka kwa Komandoo Jide ndni ya Nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam.
Hapa Lady Jay Dee akifanya mahojiano na mtangazaji mahiri wa clouds fm Millard Ayo
Gadner G. Habash ambaye ni mmoja wa Wakurugenzi wa Nyumbani Lounge na Machozi Band akizungumza na vijana walioshiriki katika kutengeneza Video mpya ya Joto Hasira ya Lady JayDee
 Prof.J ameshiriki katika wimbo huo wa Lad JayDee Joto Hasira nae alikuwepo Ukumbini hapo, hapa akipiga picha na Warembo walio pamba show hiyo.
Shangwe Za kutosha kwa Komandoo Jide
Wana dada waandishi wa habari waki show love katika uzinduzi wa wimbo wa Lady Jay Dee "JOTO HASIRA"

Wednesday, March 6, 2013

HEMEDI,TIMBULO,ROSE NDAUKA NA MZEE CHILO KUTOKA NA MOVIE YA WORLD OF BENEFIT

 Sehemu ya Movie ya World of Benefit


 Maandalizi ya utayarishaji wa Movie.




Wasanii wakiwa location kwa ajili ya Movie mpya ya WORLD OF BENEFIT.

Picha kwa hisani ya Mcddenis Mgatha

Tuesday, March 5, 2013

KWANZA RECORDS NA UJIO MPYA

Kwanza Records ni studio ya kisasa iliyopo Morogoro mjini ambayo kazi zake zimekuwa zikifanya vizuri katika uimwengu wa muziki wa kizazi kipya. Kwa mara ya Kwanza Studio ya Kwanza Records ilifanikiwa kumtambulisha katika anga la Muziki wa Bongo Fleva Msanii na Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania ajulikanaye kwa jina la Kitale akimshirikisha msanii mwenzake ambaye kwa sasa ni marehemu, namzungumzia Sharo Milionea. 

Wasanii hao kwa pamoja waliweza kutengeneza nyimbo nzuri na inayopendwa na wengi ijulikanayo kama HILI DUDE NOMA., Nyimbo hiyo imekuwa gumzo katika anga la muziki wa kitanzania. Kwa faida ya wapenzi wa Blog hii, mwasisi wa Studio ya Kwanza Records ni Amani Mwaipaja. Lengo kuu la studio ya Kwanza Records ni kusaidia vijana wa kitanzania kukuza vipaji vyao kupitia sanaa ya muziki hasa wasanii watokao mikoani.

 Mpaka sasa, baadhi tu ya wasanii walioweza kutoka kupitia studio ya Kwanza Records ni pamoja na: 
Kitale na Sharo Milionea (jina la wimbo-Hili dude noma) Asha Boko (jina la wimbo-Kibonge Mnene) Joh Maker (Mshindi wa Fiesta Nyota akiwakirisha Mkoa wa Morogoro 2012) Mash J (Mshiriki wa Fiesta Nyota 2012 kutokea Morogoro) Afande Sele (jina la wimbo-Mashikolo Mageni) Ballet Wallet (jina la wimbo-Mr. President) Kenedy Masanja (jina la wimbo-Kamba Ndefu) Sesilia Saleko (jina la wimbo-Kwepa Uterezi) Sifuni Kwaya (Wamefanya albam nzima) Mao Thobias (jina la wimbo-Kinywa) Levina Stiven (jina la wimbo-Usikate tamaa) J-Zinga jina la wimbo-Kibena) Mycoel (jina la wimbo Rudi) Vent Skills (jina la wimbo-Stay away) Swahili Genge (jina la wimbo-Red Card) Man Gao (jina la wimbo-Mama watoto) Man 2C (jina la wimbo-mzee wa kitaa) Jacca (jina la wimbo-mbiu ya mnyonge) Bon Face (jina la Wimbo-Bado mtoto) Mide Zoo Kwa ujumla list ya wasanii waliopitia kwanza Records ni kubwa na inazidi kuongezeka kila kukicha.Studio ya Kwanza Records ipo chini ya Producer Vent Skills na sasa Kwanza Records inamtambulisha kwenu Msanii Mycoel,Tafadhalini Mpokeeni Kwa mawasiliano piga 0653 361 070

Friday, March 1, 2013

NGOMA AFRICA BAND INAFANYA VIZURI UGHAIBUNI

Ngoma Africa Band, a German based Tanzanian band is now one of the oldest and most successful Africans bands in Germany.

Many African bands in Europe hardly survive for more than a year. Yet Ngoma Africa Band, founded by Ebrahim Makunja aka Ras Makunja in 1993, is still growing stronger.
The band plays "Bongo Dance", which is a unique combination of traditional and modern Tanzanian rhythms with  Soukous and Rumba. All theirs songs are in Kiswahili.
Ngoma Africa Band has released several successful hits including “Mama Kimwaga” (Sugar Mummy), “Anti-Corruption Squad” and “Apache wacha Pombe” (Stop over drinking).

In 2010 Ngoma Africa Band released a single in praise of Tanzania’s President Jakaya Kikwete. The song titled “Jakaya Kikwete 2010” praises Mr. Kikwete’s good leadership skills and commitment to fight corruption.

On 12th August 2012, Ngoma Africa Band received the International Diaspora Award (IDA) at the International African Festival Tubingen 2012, Germany, for their hard work in promoting East African music throughout Europe.

Ms. Susan Muyang Tatah, CEO of the International African Festival Tubingen 2012 said Ngoma Africa Band was also chosen for the Award because of their creative performance on stage. It’s difficult to resist dancing at their concerts, she said.
This year the band released a new CD titled "Bongo Tambarare" featuring "Supu ya Mawe" and "Uhuru wa Habari". The new release is already dominating air waves in Tanzania.

"Supu ya Mawe" advices the listeners to work hard and be patient while pursuing their objectives in life. It also appeals for generosity towards the needy.
"Uhuru wa Habari" praises African journalists who are bold enough to speak out the truth in environments where freedom of speech is quite limited.

Ngoma Africa Band is famous for staging thrilling shows in festivals in different parts of Europe. The band’s joyful female dancers, wearing traditional costumes and dancing vigorously to their tunes, always leave fans asking for more.
 
Ngoma Africa Band is composed of talented young musicians including soloist Christian Bakotessa aka Chris-B, Said Vuai, Matondo Benda, Jonathan Sousa, Aj Nbongo, Prince Zongolo, Bedi Beraca "Bella" and Jessy Ouyah.


For further information about Ngoma Africa Band and to listen to their music, please visit   www.ngoma-africa.com.
By Stephen Ogongo Ongong’a