Thursday, October 2, 2014

VITUKO VYA MASTAA ;AMBER ROSE NA WIZ KHALIFA


Amber1Kuvunjika kwa ndoa ya mastaa Amber Rose na Wiz Khalifa kumeendelea kuchukua nafasi kwenye headlines za dunia na hii ni baada ya Amber kutaja chanzo mojawapo cha kuvunjika kwa uhusiano huo.
Kwenye interview ya Radio Amber amesema kingine kilichomkasirisha ni kuona Wiz anawaendekeza warembo flani wawili mapacha ambao inaaminika amekua akijihusisha nao kimapenzi.
Amber amesema alipenda kuiokoa ndoa yake ili waendelee kuwa pamoja lakini anaeonekana kukataa kuendelea kuwa kwenye ndoa ni Wiz mwenyewe, Amber anasema hata taarifa za mwanzoni kwamba walitengana siku nyingi kabla ya kutaka talaka zilikua za uongo…. hakufanya maamuzi yao sababu alitaka kuiokoa ndoa yake. amber 2Amber amemshutumu Wiz kwa kutoka kimapenzi na hawa mapacha kwenye hii picha hapa chini…
amber 3

Wednesday, April 23, 2014

MWAIPAJA BLOG NDANI YA ULANGA

Mwanasheria Amani Mwaipaja akiwa Ndugu Mohamed Nguku ambaye ni Msaidizi wa kisheria kutoka kituo cha wasaidizi wa sheria Ulanga nje ya jengo la Chama cha Wasioona Ulanga. Mwanasheria Mwaipaja yuko wilayani Ulanga kwa ajili ya kutambulisha Mradi wa Kuboresha na kuimarisha upatikanaji wa Huduma ya Msaada wa kisheria Mkoani Morogoro, mradi wa miaka miwili unaofadhiliwa na Legal Services Facility
Mwanasheria Amani Mwaipaja akiwa na Mtangazaji wa Radio Ulanga Fm Fatma Mtemangani nje ya ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga

Wadau wa Mradi wakisikiliza maelezo kutoka kwa mwanasheria Amani Mwaipaja (Hayupo pichani) ndani ya ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga
Nje ya ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
 Mto Kilombero kipindi cha Mvua unavyoonekana





Tuesday, April 22, 2014

MTANGAZAJI MADUHU ATEMBELEA STUDIO YA KWANZA RECORDS


Mtangazaji Mkongwe kwenye Tasnia ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini Tanzania Maduhu Jumanne ( Mwenye Miwani) ambaye anafanya kazi kwenye kituo cha Radio cha Morningstar Radio na Televisheni ya Morningstar Tv inayomilikiwa na Kanisa la Waadventista Wasabato nchini Tanzania akiwa kwenye picha ya pamoja na Mtayarishaji wa Muziki wa Studio ya Kwanza Records ajulikanaye kwa jina la Vent Skillz
Mtayarishaji wa Muziki (Producer) wa Kwanza Records Vent Skillz akiwa kazini. Studio ya Kwanza Records inapatikana Morogoro Mjini ni studio maarufu na yenye mchango mkubwa katika kukuza, kuendeleza na kuibua vipaji na muziki wa Kitanzania